Jumatatu , 20th Jul , 2020

Messi wa Pichichi
Kwa msimu wa tatu mfululizo, hakuna mchezaji aliyetoa pasi za usaidizi katika LaLiga kuliko Lionel Messi.

Lionel Messi tuzo 7 za Pichichi

Messi wa Pichichi
Kwa msimu wa tatu mfululizo, hakuna mchezaji aliyetoa pasi za usaidizi katika LaLiga kuliko Lionel Messi.
Messi amehusika kutoa pasi 12 za magoli, msimu wa 2017/18, pasi 13 za magoli na pasi 21 za magoli kwa msimu huu wa 2019/20.
Muargentina huyo pia anaibuka kidedea wa ufungaji kwa msimu huu kwa kufunga mabao 25 na anachukua tuzo ya pichichi mara ya 7 ikiwa ni mara nyingi zaidi
Maajabu ya Thibaut Courtois
Thibaut Courtois anakuwa mlinda mlango wa kwanza kutwaa tuzo ya Zamora akiwa na vilabu viwili vya mji wa Madrid.
Courtois aliruhusu mabao 20 tu katika mechi 34 za ligi akiwa na mabingwa wa La Liga Real Madrid.
Courtois alikuwa na wastani mzuri wa 0.59 kwa kila mchezo, akiwafunika Jan Oblak wa Atletico Madrid mwenye 0.64 wastani na Unai Simon wa Bilbao wastani wa 0.84 kwa kila mchezo.
Courtois mwenye umri wa miaka 28 alichukua tuzo ya Zamora pia akiwa na Atletico Madrid kwa misimu miwili huko nyuma.
Mbelgiji huyo anaingia kwenye orodha ya walinda mlango 11 wa Real Madrid waliochukua tuzo hiyo.
Sergio Ramos beki mfungaji
Mlinzi huyo wa kati wa Real Madrid anamaliza msimu wa La Liga kwa kufunga mabao 11, ikiwa ni rekodi kubwa beki kufikisha idadi hiyo.
Hapo nyuma mlinzi Mariano Pernia alishikilia rekodi hii kwa mabao yake 10 akiwa na Getafe miaka 15 iliyopita.