Jumatano , 11th Mei , 2022

Timu za Miami Heat na Phoenix Suns zinahitaji ushindi mmoja katika michezo 2 ya mtoano (playoffs) iliyosalia ya hatua ya nusu fainali kwenye muendelezo wa michezo ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA ilikujihakikishia tiketi ya kufuzu fainali.

Jimmy Butler ameiongoza Miami kushinda game 5 dhidi ya Philadephia 76ers Amefunga alama 23

Ukanda wa Mashariki Miami Heat wameshinda mchezo wa 5 (game 5) leo Alfajiri dhidi ya Philadephia 76ers kwa alama 120 kwa 85 na sasa Miami wanaongoza  kwa 3-2 kwenye mfululizo wa michezo 7 ya nusu fainali.

Katika mchezo huu mchezaji nyota wa Miami Jimmy Butler amefunga alama 23, pasi za kufunga (Assists) 6 na Rebound 6. Na Emmanuel Embiid wa 76ers hakuwa na game nzuri amefunga alama17 pasi za kufunga (Assist) 2 na Rebound 5.

Ukanda wa Magharibi mchezo wa 5 (game 5) ya nusu fainali Phoenix Suns wameinyuka Dallas Mavericks kwa alama 110 kwa 80. Nyota wa Suns Davin Booker amefunnga alama 28, pasi za kufunga (Assists) 2 na rebound 7. Luka Doncic wa Mavericks amefunga alama 28, pasi za kufunga (Assists) 2 na rebound 11. Mchezo wa 6 (Game 6) inachezwa kesho Mei 12, 2022.