Jumanne , 1st Mar , 2022

Mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Copa Italia inachezwa leo usiku ukiwa ni mchezo wa mkondo wa kwanza ambapo AC Milan watakuwa wenyeji wa Inter Milan katika dimba la San Siro. Hii ni derby ya jiji la Milan ikiwa ni kwa mara ya 26 timu hizi zinakutana kwenye michuano hii.

(Mshambuliaji wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic katika harakati za kuwahi mpira katika moja ya Milan Derby)

Kuelekea mchezo huu Kocha wa AC Milan Stefano Pioli atakosa huduma ya kiungo Sadro Tonali ambaye anatumikia adhabu na Zlatan Ibrahimovic ambaye bado hajapona majeruhi, kwa upande wa inter Milan kocha Simone Inzaghi hana wachezaji wenye majeraha na Matias Vecino atakuwa akirejea baada ya kuumia wiki iliyopita pamoja na Robin Gonsens aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo anatarajiwa kuwa sehemu ya mchezo.

(Kombe la michuano ya Coppa Italia)

Msimu uliopita timu hizi zilikutana hatua ya robo fainali kwenye michuano hii na Inter Milan walifanikiwa kuitoa AC Milan kwa kuinyuka kwa mabao 2-1. Lakini msimu huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu AC Milan waliifunga Inter Milan 2-1. Mchezo wa nusu fainali ya pili utachezwa kesho ambapo Fiorentina watacheza dhidi ya Juventus.