Ijumaa , 17th Jul , 2020

Klabu ya soka ya Mbao imeandikisha rekodi mpya katika ligi kuu ya kuwa timu ya kwanza msimu huu kushinda mechi tano mfululizo na kuendelea kusalia katika nafasi ileile waliyokuwepo awali.

Kocha wa Mbao Fc ya Mwanza, Fredy Felix Minziro (pichani) katika moja ya mahojiano na EATV.

Mbao ilishinda dhidi ya Polisi Tanzania kwa bao 1-0, ikainyuka Lipuli Fc bao 2-0, ikailaza Mtibwa Sugar bao 1-0, ikainyoosha Coastal Union bao 1-0 na jana ikawaadhibu mabingwa watetezi kwa bao 3-1.

Kabla ya hapo Mbao ilikua katika nafasi ya 18 katika msimamo wa VPL,lakini licha ya kukusanya alama 15 katika michezo hiyo mitano,bado imeendelea kusalia hapo hapo wakiwa na alama 38.

Ingizo jipya la kocha Fredy Felix Minziro ndilo lililotea mabadiliko ya moja kwa moja katika kikosi hicho, na zifuatazo ndizo takwimu za kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Yanga,Kmc na hata Sinngida United.

REKODI ZA MINZIRO

Tangu achukue mikoba kukinoa kikosi hiko hajapoteza mechi yoyote.
.
Mechi-5
Ushindi-5

-Ndiye Kocha wa kwanza Mbao Fc kushinda match 5 mfululizo msimu huu.
-Kocha wa kwanza wa Mbao Fc aliyeweza kuifunga Simba sc goli nyingi 3.

-Klabu ya kutoka Mwanza , ambayo haijapoteza mchezo wowote katika michezo 5 mfululizo tangu kocha Minziro achukue timu.

MATOKEO YAO KATIKA MECHI 5 ZILIZOPITA

1 Mbao 1-0 Coastal Union
2.Mbao fc 1 - 0 Polisi Tanzania
3. Mbao fc 2 - 0 Lipuli fc
4.Mbao fc 1 - 0 Mtibwa sugar
5. Simba sc 2 - 3 Mbao fc