Jumatano , 23rd Jun , 2021

Kocha wa Sevilla Julen lopetegui naye ameikataa ofa ya kuifundisha Tottenham ya Uingereza baada ya kuombwa kujiunga nayo ,kama ambavyo makocha wengine Antonio Conte,Paulo Fonseca Ganaro Gattuso walivyofanya.

kocha Julen Lopetegui

Kwa mujibu wa Rais wa klabu ya Sevilla Jose Castro amesema’’ Ni kweli Tottenham walimuhitaji kocha wetu lakini alikaataa kwa kuwa ana furaha kufanya kazi mahala hapa na pia mapenzi ya dhati na timu yetu ‘’

Tottenham imekuwa bila kocha kwa muda sasa tangu Jose Mourinho atimuliwe mwishoni mwa mwezi aprili kutokana na mwenendo mbaya ya matokeo.

Mwenyekiti wa timu hiyo Daniel Levy amekuwa akihaha kutafuta mbadala wa Mourinho bila mafanikio, makocha wengi wamehusishwa kujiinga Tottenham lakini hakuna dili iliyokamilika hadi sasa wakati ambapo timu zinajiandaa na maadalizi ya msimu.