
Wakiwa wametoka kushinda dhidi ya Mbeya City, Wanamangushi Coastal Union itashuka dimbani dhidi ya Mtibwa Sugar iliyotoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania.
Mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa utachezwa Uwanja wa Mkwakwani,Tanga.
Pia KMC itashuka Uwanja wa Azam Complex ambapo itamenyana na Ruvu Shooting iliyojeruhiwa bao 4-1 kwenye mchezo ulipita dhidi ya Azam FC.
Ikumbukwe kwamba jana Desemba 27 kulikuwa na mechi ambazo zilichezwa na baada ya dakika 90 mambo yalikuwa namna hii:-
Geita Gold 1-1 Mbeya Kwanza Uwanja wa Nyankumbu.
Polisi Tanzania 0-0 Mbeya City, Uwanja wa Ushirika, Moshi.