Alhamisi , 5th Mei , 2022

Andy Murray amejiondoa kwenye mchezo wake dhidi ya Novak Djokovic kwenye michuano ya wazi ya Madrid kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa.

Novak Djokovic (kulia) na Andy Murray(kushoto) kwenye picha ya pamoja.

Raia huyo wa Uingereza alipangwa kucheza na Djokovic leo kwenye raundi ya tatu ya michuano hiyo lakini imeshindikana na hii ni kwa mujibu wa ripoti ya waandaaji wa mashindano.

Murray ambaye anashikilia nafasi ya 78 kwenye viwango vya ubora alimchapa bingwa wa michuano ya wazi ya Marekani mwaka 2020, Dominic Thiem kwenye raundi ya kwanza kabla ya kumbwaga Denis Shapovalov katika raundi ya pili.

Ilikuwa ni fursa kwa Murray kukutana na Djokovic ambaye wamekua pamoja na wameshakutana mara 36 kwenye mashindano mbalimbali.