Jumanne , 18th Jan , 2022

Mwamuzi wa Tanzania Frank Komba ni miongoni mwa waamuzi watakao chezesha mchezo wa kundi C wa michuano ya AFCON mchezo kati ya timu ya taifa ya Gabon dhidi ya Morocco, mchezo unaochezwa leo Saa 4:00 Usiku katika muendelezo wa michuano hii inayoendelea nchini Cameroon.

Frank Komba

Franka Komba kwenye mchezo huu atachezesha kama mwamuzi msaidi namba 2, akimsaidia mwamuzi wa kati  Dahane Beida kutoka Mauritanian mwamuzi msaidizi namba 1 ni Attia Amsaad kutoka Libya na mwamuzi wa akiba (fourth referee) ni Maguette Ndiay kutoka Senegal.

Komba ni mwamuzi pekee kutoka Tanzania aliyeorodheshwa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF kuchezesha michuano hii ya mataifa barani Afrika, na kabla ya kuanza kwa michuano hii Komba aliiambia EATV kuwa moja ya ndoto yake kwenye kazi ya uamuzi wa mpira wa miguu ilikuwa ni kuchezesha kwenye michuano hii mikubwa kwa ngazi ya timu za taifa barani Afrika.

Mchezo wanaochezesha usiki wa leo unaowakutanisha vinara wa Kundi C timu ya taifa ya Morocco ambao wana alama 6 na tayari wameshafuzu hatua ya 16 bora, dhidi ya Gabon ambao wapo nafasi ya pili kwenye kundi hilo wakiwa na alama 4 wakihitaji sare kwenye mchezo huo ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua inayofaya ya 16 bora.

Mchezo mwingine wa kundi hilo Ghana wenye alama 1 wanaminyana na Comoro ambao hawana alama hata moja na ndio wanaburuza mkia kwenye kundi C.