Ijumaa , 13th Mei , 2022

Nahodha wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto amesema bado ubingwa huko wazi kwao na nilichotokea kwenye mechi tatu mfululizo ni upepo tu ambao huvuma na kutulia.

Nahodha wa Yanga Baraka Mwamnyeto.

Maneno hayo yamesemwa na nahodha Mwanyeto kuwa wanakwenda Dodoma kuchukua pointi tatu ili kurudisha furaha kwa mashabiki wao.

"Tunahitaji kuondoa gundu la droo kwenye mechi tatu mfululizo, hivyo tunakwenda Dodoma na nguvu na ari mpya ya kupata matokeo mazuri," amesema Mwanyeto .

Kuhusu walichokiboresha kwenye kikosi chao baada ya sare mfululizo, Mwamnyeto amesema kilichotokea ni upepo tu wa mpira, wako vizuri na wanaamini watapata ushindi mnono kwenye mchezo huo.

"Katika maisha kuna wakati wa raha na shida, hata maandiko matakatifu yanatueleza hivyo, hivyo Yanga tulipitia kwenye raha, sasa ni wakati wa shida lakini naamini tutatoka hapa tulipo na kuwa kwenye raha zaidi siku si nyingi," amesema.

Kuhusu safari ya ubingwa, mchezaji huyo amesema bado ipo kwa Yanga kutokana na tofauti ya pointi walizonazo mpaka sasa dhidi ya Simba, ubora wa kikosi chao na hamasa ya timu msimu huu.