Jumanne , 6th Sep , 2022

Mzunguko wa 3 wa Ligi Kuu Tanzania Bara(NBC Premier League 2022/23) inarejea leo kwa michezo miwili kuchezwa baada ya kusimama kwa wiki mbili kupisha michezo ya Taifa Stars ya kuwania kufuzu fainali za CHAN 2023 nchini Algeria.

(Wachezaji wa Yanga Bakari Mwamnyeto na Fiston Mayele wakizuiliwa na mlinzi wa Azam FC Abdallah Kheri Sebo)

Mchezo wa kwanza leo unachezwa Saa 10:00 jioni katika Dimba la CCM Kirumba Mwanza ambapo Geita Gold FC watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar, Timu hizi zinatofautiana alama 1 tu huku Geita wakiwa nafasi ya 13 na alama 1 na Kagera Sugar wanakamata nafasi ya 16 wakiwa hawana alama.

Mchezo wa Pili leo utakuwa ni Mzizima Dabi baina ya Yanga dhidi ya Azam FC kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam, mchezo huu utachezwa Saa 1:00 usiku. Timu hizi zinaelekea kwenye mchezo huu zikiwa zinatofautiana alama 4 tu kwenye msimamo wa Ligi, Yanga wakiwa nafasi ya 2 na alama 6 ilhali Azam FC wana alama 4 wakiwa nafasi ya 5.

Yanga kuelekea mchezo wa leo huwenda wakakosa huduma ya mlinzi Djuma Shaaban aliyekuwa anaumwa Malaria na Golikipa Djigui Diarra aliyekuwa majeruhi lakini jana walifanya mazoezi jna wenzao huku upande wa Azam FC watawakosa huduma ya nyota watatu kutokana na majeruhi ambao ni Rodgers Kola, Kenneth Muguna na Aziz Kadar.