Jumatatu , 9th Mei , 2022

Michezo miwili ya nusu fainali kwenye mitoano ya ligi kuu ya kikapu nchini Marekani ziliendelea Asubuhi kwa timu za Philadelphia 76ers na Dallas Mavericks kupata ushindi na kufanya michezo yao kuwa 2-2 kati ya mechi 4 za NBA walizokutana.

Joel Embiid akionyesha umahiri wake

76ers iliosheheni nyota kama James Harden aliyefunga vikapu 31 na Joel Embiid aliandika mlama 24 ilitosha kuwapa ushindi Philadelphia kwa vikapu 116-108 Mbele ya Miami Heats katika dimba la Wells Fargo center Philadelphia.

Miami waliifunga 76ers katika michezo miwili ya mwanzo iliyocheza Miami, Florida huku wakizidiwa maarafa baada ya kurejea kwa Joel Embiid kwenye michezo miwili iliyochezwa Philadelphia, Pennsylvania.

Dallas Mavericks waneonesha makali yao dhidi ya Phoenix Suns baada ya kuilaza Kwa vikapu 111-101 katika uwanja wa America airlines center.

Luka Doncic alitumia faida ya uwanja wa nyumbani kwa kufunga alama 26 huku Dorian Lawrence Finney-Smith aking'ara kwa kufunga alama 24 na kufanya timu hizo mbili kufungamana 2-2 katika michezo 7 ya nusu fainali.

Phoenix hawakuwa na usiku mzuri baada ya nyota wao kufanya madhambi mengi dhidi ya Dallas na kuwafanya kucheza kwa tahadhali zaidi kuepuka adhabu ya kutolewa kiwanjani.

Michezo wa kukata na shoka utapigwa usiku wa kuamkia kesho, Memphis Grizzlies watakuwa ugenini dhidi ya Golden State Warriors huku timu zenye safu bora ya ulinzi za Milwaukee Bucks itamenyana na Boston Celtics.