Alhamisi , 17th Nov , 2016

Uongozi wa Ndanda FC umesema, utahakikisha unafanya usajili wa wachezaji wenye vipaji ili kuweza kuwa vizuri zaidi katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.

Ndanda FC wakichuana dhidi ya Yanga Uwanja katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam msimu uliopita.

 

Afisa habari wa Ndanda FC Idrisa Bandari amesema, kikosi hakikuwa katika hali mbaya katika mzunguko uliopita japo kulikuwa na mapungufu yaliyokuwa yakijitokeza na ripoti ya kocha pia inaonesha kunahitajika marekebisho hivyo wameona ni vizuri kusajili kutokana na mapendekezo ya kocha ili kukijenga zaidi kikosi hicho.

Bandari amesema, mpaka sasa wapo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji ambao wanaamini wataweza kuisaidia timu ya Ndanda katika michuano ya ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

Bandari amesema, mara baada ya kumaliza usajili ambao wanaamini utakiimarisha kikosi zaidi, kikosi hicho kitaelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Desemba 17 mwaka huu.