Jumatatu , 20th Mei , 2019

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amempongeza nahodha wa taifa Stars Mbwana Samatta, kwa kutwaa ubingwa wa soka Ubelgiji na klabu yake ya KRC Genk.

Zitto Kabwe

Zitto ambaye ni shabiki mkubwa wa soka akishabikia klabu za Simba na Liverpool amesema, Tanzania inahitaji watu kama Samatta wengine 100 ili kusaidia kulitangaza taifa letu kimataifa.

Zitto ametumia Instagram kueleza hayo akiweka wazi kuwa video ya mashabiki wa Genk wakishangilia na bendera ya Tanzania ni kitu kikubwa kwa taifa. ''Hii ni free advert ya nchi. Hapa ni Genk ambapo @samagoal77 anacheza. We need hundreds of Samatta nje''.

Aidha Zitto ameeleza namna ambavyo Nigeria inapata faida kama hizo kutokana na kuwa na wachezaji wengi Ulaya. ''Fikiria Nigeria wanapata Remittances kiasi gani kutoka exports ya wachezaji wao kwenye ligi za Ulaya na penginepo.

Mashabiki wa Genk na Samatta wakipeperusha bendera ya Tanzania kwenye uwanja wa Cristal Arena.

Pia amemshukuru Samatta kwa kusema ''Asante sana Mbwana Samatta kwa heshima hii kwa nchi yetu''.

Samatta akiwa na Genk amefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya huko huku akimaliza akiwa kinara wa magoli baada ya kufunga mabao 20 kwenye msimu wa 2018/19.