
Mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe
Mbappe mwenye umri wa miaka 23 aliyeongeza kandarasi mpya ndani ya klabu ya PSG mpaka 2025 amesema alikutana na maofisa wa klabu ya Liverpool miaka 5 iliyopita akiwa bado anacheza katika klabu ya Monaco mnamo mwaka 2017.
"tulifanya mazungumzo japo hayakuwa marefu, Liverpool ni klabu kubwa na yenye historia ndani yake lakini pia mama yangu anaipenda klabu hiyo na sijui kwanini anaipenda klabu hiyo kwa maana mnapaswa kumuuliza yeye mwenyewe lakini mwishoni ilikuwa nichague kucheza kati ya Real Madrid au Paris Saint Germain ”amesema Mbappe
Vilabu vya Real Madrid na Liverpool watacheza mchezo wa fainali wa kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya(Uefa Champions League) kwa msimu wa 2021/22 mnamo Mei 28,2022 kwenye jiji la Paris,Ufaransa