Jumamosi , 2nd Sep , 2017

Kamishna wa Ufundi na Mipango ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Manase Zablon amesema anaimani kubwa katika fainali ya leo ya Sprite BBall Kings (game 5) kwamba ataweza kupatikana bingwa wa kweli bila ya shaka yeyote ile kwa mashabiki.

Kamishna wa Ufundi na Mipango ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Manase Zablon.

Manase ameeleza hayo ikiwa yamebakia masaa kadhaa vumbi kutimka katika michuano hiyo ambayo kwa siku ya leo ndiyo itaweza kumtambulisha bingwa kwa mwaka 2017 baada ya timu ya TMT na Mchenga BBall Stars zote kwa pamoja kulingana kwa matokeo yao ya awali ambapo kila timu imefungwa mara mbili na kushinda mara mbili. 

"Nina imani kabisa katika mchezo wa leo wa fainali za Sprite BBall Kings, tutapata bingwa aliyekuwa halali na fainali itakuwa nzuri. Niwaombe Watanzania wote mjitokeze kwa wingi kuja kushuhudia fainali ya aina yake", alisema Manase. 

Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Sprite BBall Kings anatarajiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni 10 akifuatiwa na mshindi wa pili kupata milioni tatu bila ya kumsahau mchezaji bora {MVP} kuondoka na shilingi milioni mbili.