Jumamosi , 1st Oct , 2022

Klabu ya  Simba itakosa huduma ya wachezaji wake 3 kuelekea mchezo wa mzunguko wa 5 wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/23 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kuelekea mchezo huo,Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema ziara ya siku 6 visiwani Zanzibar kumewapa matayarisho mazuri huku wakikosa huduma ya wachezaji 3 kuelekea mchezo wa kesho

“Kuna wachezaji tutawakosa Kapombe (Shomari) ana majeraha,Banda (Peter) aliumia kwenye michezo ya kirafiki Zanzibar na Sakho(Pape Ousmane) ana matatizo ya kifamilia kwani alipata msiba,tunajua mchezo hautakuwa mwepesi lakini tumejipanga kupata matokeo kesho”amesema  Selemani Matola 

Baada ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Kikosi cha Simba inataraji kusafiri kuelekea nchini Angola kwa ajili ya mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Primiero de Agosto utakaochezwa Jumapili ya Oktoba 9, 2022.