Alhamisi , 21st Apr , 2022

Manguli wa zamani wa ligi kuu ya England akiwemo Sergio Kun Aguero, Paul Scholes, Vincent Kompany, Didier Drogba, Ian Wright na goli kipa Peter Schmeichel wameingizwa kwenye orodha ya watakao wania tuzo ya heshima ya ligi hiyo “Hall of Fame”.

(wanao wania tuzo ya heshima ligi ya England 2022)

Sababu tofauti za kila mmoja ndio zimewafanya maguli hawa kutajwa katika tuzo hizi za heshima, wakati Sergio Kun Aguero akiwa ndiye mchezaji wa kigeni aliyefunga mabao mengi zaidi kwa wachezaji wasio raia wa England katika historia ya Ligi hiyo akifunga magoli 184. Paul Scholes alishinda mataji 11 ya ligi kuu ya England akiwa na Manchester Utd. Vicent Kompany aliisaidia Manchester City kuwa na nguvu kubwa ya upinznai wa kweli katika ligi hiyo.

Didie Drogba alishinda mara nne ubingwa wa ligi kuu ya England akiwa na Chelsea huku Ian Wright alifanikiwa kufunga mabao 113 ya EPL na Peter Schmeichel akiwa ndio goli kipa wa kwanza kuingizwa katika kuwania tuzo hizo za heshima.

Magwiji hawa Wanaungana na Wayne Rooney na Patrick Vieira kama wachezaji wa wasio na muda mrefu zaidi tangu kustaafu kwao walioingia kwenye wachezaji waliopendekezwa kushinda tuzo hizo za heshima za Ligi ya England, na kufikia jumla ya wachezaji 16.

(waliopendekezwa kabla ya mchujo kwenye tuzo za heshima ligi kuu ya England)

Uamuzi wa kuchagua wachezaji hawa ulitokana na kura za mtandaoni zilizopigwa hadharani na Jopo la wasimamizi wa Tuzo za Ligi Kuu, wakiambatanisha na tuzo hizi za heshima zikiwatambua wachezaji bora waliotamba kwenye ligi hiyo tangu ilipobadilishwa jina mwaka wa 1992.

Tuzo hizi za heshima kwa wachezaji wa zamani wa ligi kuu ya England, zilizinduliwa mwaka wa 2021, huku Thierry Henry na Alan Shearer wakipata tuzo hizi wakiwa wa kwanza. Kisha David Beckham, Dennis Bergkamp, Eric Cantona, Steven Gerrard, Roy Keane, na Frank Lampard walkafatia kukamilisha orodha ya tuzo ya heshima kwa mwaka 2021, na mapema mwaka huu Wyne Rooney na Patrick Vieira wakafungua mwaka 2022 wakipata tuzo hizo wakiwa wa kwanza kwa mwaka huu.