Jumatatu , 20th Jul , 2015

Timu ya Khatoum ya Sudan imeifunga timu ya Telecom ya Djibout magoli 5-0,katika michuano ya klabu bingwa kwa nchi za Afrika Mashariki na kati 'kombe la kagame'inayoendelea jijini Dar es salaam.

Michael Olunga

Timu ya Khatoum ya Sudan imeifunga timu ya Telecom ya Djibout magoli 5-0,katika michuano ya klabu bingwa kwa nchi za Afrika Mashariki na kati 'kombe la kagame'inayoendelea jijini Dar es salaam.

Magoli ya Khatoum yamefungwa kwa Penati na Salah Osman dakika ya 22 na 37, la tatu likipachikwa na Ousmaila Baba dakika ya 67, Awad Abdallah amefunga goli la nne dakika ya 81,na la goli la tano limefungwa na Murwan Abdallah.

Katika mchezo wa pili timu ya Gor Mahia ya Kenya imeifunga KMKM mabao 3-1 magoli mawili kati ya matatu ya Gor Mahia yamefungwa na Michael Olunga ambaye pia ndiye aliyewanyoa Yanga katika mchezo wa kwanza na kufikisha point 6 katika kundi A.

Katika michezo ya timu hizo iliyopita, Gor Mahia iliifunga Yanga Goli 2-1, Nao KMKM iliichabanga Telecom goli 1-0.

Michuano hiyo itaendelea kesho ambapo Al Ahly Shandy ya Sudani itacheza na LLB AFC ya Burundi saa 8:00 mchana uwanja wa Taifa, na kufuatia na mchezo kati ya Heegan FC ya Somalia na APR ya Rwanda saa 10 katika uwanja wa Karume wakati Azam FC ikiikabili Malakia ya Sudan Kusini saa 10:00 katika dimba la Taifa.