Jumatatu , 31st Mei , 2021

Michezo ya mtoano hatua ya nusu fainali ya ligi ya kikapu nchini Marekani 'NBA Playoff' inatazamiwa kuendelea usiku wa kuamkia kesho kwa michezo miwili, Washington Wizard watacheza dhidi ya Philadelphia 76ers saa8:30 usiku ilhali Memphis Glizzlies watakipiga na Utah Jazz saa 11:00 Alfajiri

Joel Embid wa Philadelphia 76ers akijaribu kutupia mpira.

Philadelphia 76ers wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na uongozi wa michezo yote mitatu iliyopita huku wakisaka ushindi mmoja tu kufuzu hatua ya nusu fainali na kuwatupa nje Washington Wizard ambao hawajashinda hata mchezo mmoja.

Mchezo mwingine ni ule utakaowakutanisha Memphis Glizzlies dhidi ya Utah Jazz ambapo Utah anaongoza akiwa na ushindi wa michezo miwili huku Glizzlies wakiwa na ushindi kwenye mchezo mmoja tu. Ili mmoja kati ya wawili hao afuzu hatua inayofuata ya Nusu fainali atalazimika kushinda jumla ya michezo minne.

Kwa matokeo ya michezo iliyochezwa usiku wa kuamkia leo;

Timu ya Brooklyn Nets iliibuka na ushindi wa alama 141 mbele ya Boston Celtics ambao walipata alama 126 kwenye mchezo wa mtoano wa robo fainali ya ligi hiyo na kuongoza kwa jumla ya michezo 3 kwa 1 hivyo akiibuka na ushindi mmoja basi atafuzu nusu fainali.

Kwenye mchezo huyo, Kevin Durrants ameibuka kuwa nyota wa mchezo kwa kupata alama 42, rebaundi 4 na assisti 5. kwenye mchezo mwingine, Los Angeles Clippers wamepata ushindi wa alama 106 kwa 81 dhidi ya Dallas Mavericks na kufanya matokeo yao kuwa sare ya 2-2.