(Kikosi cha Polisi Tanzania msimu wa mwaka 2021-2022)
Kuelekea mchezo huo, Polisi Tanzania imesafiri na wachezaji 24 na viongozi 7 pamoja na benchi la ufundi na kumuacha Dodoma beki wake wa kati Saidi Juma ‘Makapu’ mwenye majeruhi.
Makapu aliumia kwenye mchezo dhidi ya Geita mchezo uliomalizika kwa Polisi kukubali kipigo cha kwanza kikubwa tangia kupanda ligi kuu baada ya kupoteza kwa 3-1 katika uwanja wa Nyankumbu.
Wachezaji watatu waliokuwa na majeraha kipa namba moja Metacha Mnata, beki wa kushoto Yahaya Mbegu na kiungo mshambuliaji Rajabu Athumani waliungana na timu na kufanya mazoezi ya pamoja huku Tariq Seif na Deusdedity Cosmas Okoyo wameendelea kusalia nyumbani Moshi wakiendelea na matibabu ya majeraha waliyoyapata.
Katika mchezo wa mwisho uliozikutanisha Polisi Tanzania na Tanzania Prison katika uwanja wa Ushirika, Polisi walichomoza na ushindi wa goli moja mbele ya mashemeji zao likifungwa na Tariq Simba.

