Alhamisi , 26th Aug , 2021

Ligi kuu ya soka nchini England Premier League imepanda na kuwa namba moja kwenye viwango vya ubora barani Ulaya.

Mabingwa wa Soka barani Ulaya Chelsea ya England

Viwango hivyo ambayo vimetolewa na Shirikisho la Soka barani Ulaya vimeonyesha imeishuka Ligi kuu ya Hispania La Liga ambayo sasa imeshika namba mbili.

Wakati huo Ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1 imeshuka hadi nafasi ya 6 huku Ligi kuu ya Ureno #PrimeiraLiga ikipanda hadi namba 5.

Orodha kamili kwa mpangilio

1. Premier League 
2. La Liga 
3. Serie A 
4. Bundesliga 
5. Primeira Liga 
6. Ligue 1