
Kocha wa The Blues, Thomas Tuchel akijibu maswali ya Waandishi wa Habari za michezo, baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya West Ham United, alithibitisha kuondoka kwa Chelsea
Rudiger anaondoka stamford bridge baada ya kushindwa kufikia makubaliano kutokana na kizuizi ambacho Chelsea wamekumbana nacho kutokana na sababu za kisiasa zinazomkabili mmiliki wao Roman Abramovich.
Raia huyo wa Ujerumani anaondoka Chelsea akiwa ameshinda mataji yote muhumi na matajiri hao wa jiji wa London, Ligi ya mabingwa 2021, UEFA Super Cup 2021, Klabu bingwa Dunia 2021, UEFA Europa Cup 2019 pamoja na FA Cup 2018.
Rudiger amekataa ofa za vilabu kama Juventus, Barcelona na PSG na amekuwa akiwindwa na Madrid kwa miaka mingi tangu akiwa kijana mdogo akiitumikia klabu ya Stuttgart ya ujerumani 2012-2016.
