Rekodi za leo kwenye ligi kuu ya England

Jumapili , 6th Oct , 2019

Michezo mitatu ya ligi kuu soka nchini England imemalizika jioni hii ya Oktoba 6, 2019, ambapo mabingwa watetezi, klabu ya Man City wamepoteza mchezo wa pili msimu huu.

Pep Quardiola

Man City ambao walikuwa nyumbani kwenye uwanja wa Etihad wamekubali kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa Wolves.

Kwa matokeo hayo sasa wamepoteza mechi bila kufunga goli kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa nyumbani tangu March 2016 walipofungwa na Man United 0-1 na kocha alikuwa Manuel Pellegrini.

Katika mechi nyingine Chelsea wameshinda goli 4-1 ugenini dhidi ya Southampton.

Katika mchezo huo Chelsea imeweka rekodi ya kuwa timu ya tatu kwenye historia ya EPL kufunga magoli matatu au zaidi kipindi cha kwanza ugenini kwenye mechi mbili mfululizo. Nyingine ni Manchester United msimu wa 1993/94 na Tottenham Hotspur msimu wa 2018/19. 

Katika mchezo mwingine Arsenal wameshinda 1-0 dhidi ya Bournemouth.

Katika mchezo huo Arsenal wameweka rekodi ya kuwa timu ya tatu kushinda mechi nyingi (17) kwenye uwanja wa nyumbani chini ya kocha Unai Emery tangu ulipoanza msimu uliopita. Liverpool (21) na Man City (20) wameshinda zaidi.