Ripoti ya ubora wa uwanja utakaochezewa fainali

Ijumaa , 31st Jul , 2020

Utata uliokuwepo na kuzua sintofahamu kwa wanasoka mkoani Rukwa juu ya kusuasua kwa ukarabati wa uwanja wa mpira wa Nelson Mandela umemalizwa na Chama cha soka mkoani huo pamoja na TFF.

Uwanja wa Nelson Mandela

Uwanja huo unatarajiwa kutumika katika mchezo wa fainali ya kombe la Azam Sports Federation utakaohusisha timu ya Simba Sport Club na Namungo FC.

Akithibitisha hilo Mwenyekiti wa RUREFA Blass Kihondo, amesema wana Rukwa hawana sababu ya kuwa na wasiwasi tena kwani mtaalamu kutoka TFF amejiridhisha na kusema uwanja huo upo vizuri na tayari kwa kutumika Julai 2, 2020.

Ili kuepukana na udanganyifu na wizi wa tiketi Kiondo amesema wameandaa mpango mkakati mzuri ili kuhakikisha hautokei na mchezo utaanza na kumaliza vizuri.

Tazama Video hapo chini