Ronaldo kutengwa na wenzake sababu hizi hapa

Alhamisi , 13th Mei , 2021

Cristiano Ronaldo ameripotiwa kutengwa katika chumba cha kubadilishia nguo cha Juventus na wachezaji wenzake wakiamini kwamba nyota huyo wa Ureno ana uhuru mwingi zaidi kuliko wao.

Nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo kwenye moja ya mchezo wa Serie A.

Ronaldo alifunga bao lake la 100 kwa kibibi kizee hicho cha Turin katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Sassuolo usiku wa jana ushindi ambao unamfanya Andrea Pirlo kuwinda nafasi ya nne bora, ingawa bado wanahitaji Napoli wafungwe kwenye moja ya michezo yao miwili ya mwisho.

Baada ya kipigo cha 3-0 nyumbani dhidi ya AC Milan Jumapili, wachezaji wenzake walipelekwa mazoezi lakini Ronaldo alipewa siku ya kupumzika na kwenda kukamilisha dili yake mpya ya Pauni milioni 1.4 ya Ferrari Monza huko Maranello, hali ambayo imesababisha wachezaji wengine kuto furahia ndani ya kambi ya Juventus.