Jumatatu , 30th Aug , 2021

Beki wa kimataifa wa Ureno, Ruben Diaz amerefusha kwa mwaka mmoja Mkataba wa kuendelea kusalia Manchester City hadi mwaka 2027.

Ruben Dias (pichani) mara baada ya kusaini Mkataba na Manchester City

Dias mwenye umri wa miaka 24,ambaye ndiye beki bora wa msimu barani Ulaya,na pia alitwaa tuzo ya mchezaji bora katika EPL, alisajiliwa kwa dau la Paundi Milioni 65 kwa Mkataba wa miaka 6 akitokea Benfica .

Katika msimu wake wa kwanza akiwa na Manchester City ,alionyesha kiwango kizuri na kuisaidia The Citizen kuwa na safu bora ya ya ulinzi iliyoisaidia kutwaa Ubingwa wa EPL.

Nyota huyo alitengeneza muunganiko bora katika idara ya ulinzi ya kati akiwa na John Stones ambaye pia hivi karibuni alisaini Mkataba wa kuendelea kuitumikia Manchester City.