Jumanne , 9th Mar , 2021

Michuano ya AFCON kwa timu za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 17, iliyokuwa ifanyike nchini Morocco, kuanzia Machi 13 mpaka Machi 31 mwaka 2021 imefutwa.

Sehemu ya kikosi cha Serengeti Boys

Shirikisho la Soka Barani Africa (CAF) limesema kuwa sababu ya kufuta michuano hiyo ni hofu ya janga la Corona ambapo Morocco ni miongoni mwa nchini zinazotajwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi.

Kikao cha dharura cha kamati ya utendani ya Shirikisho hilo, kimetoa maamuzi hayo, huku baadhi ya timu ikiwemo Tanzania na Uganda, zikiwa tayari zimewasili Morocco.

Kikosi cha Timu ya Taifa U17 (Serengeti Boys) kiliwasili Casablanca, Jumapili Machi 7, 2021 ambapo pia kilicheza mchezo wa maandalizi dhidi ya timu ya vijana ya Uganda na pia kilitakiwa kucheza na wenyeji Morocco kama sehemu ya maandalizi.