
‘’Lucho, nguvu na bidii yako uwanjani havitasahaulika. Ilikuwa bahati na heshima kubwa kuwa na wewe Liverpool.
Ulikuwa mchezaji mwenzetu na zaidi ya rafiki kwetu.
Tuliona jinsi ulivyopambana na kubaki imara kwenye nyakati ngumu. Uvumilivu wako ni mfano wa kuigwa na unastahili heshima kubwa.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako mpya. Endelea kuwafanya watu wako wa Colombia wajivunie uwepo wako’’ Aliandika Mohamed Salah