Jumanne , 15th Nov , 2016

Maafisa wa San Marino wametaka kuombwa radhi na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ujerumani, Thomas Muller, aliyeongea maneno ya dharau kufuatia ushindi wa mabao 8-0, Ijumaa iliyopita katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia,  mwaka 2018 nchini Urusi.

Thomas Mueller

Muller amesema kucheza na timu ya wachezaji wa ridhaa, kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia, kuliiweka Ujerumani, kwenye hatari ya kuumia, huku pia Mtendaji Mkuu wa klabu ya Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge, akisema kuwa San Marino haifanyi kitu kwenye soka la kulipwa.

Waziri wa Utalii na Michezo wa San Marino, Teodoro Lonfernini, ametaka kuombwa radhi kwa maneno hayo, na kusema Ujerumani ni mabingwa wa dunia, lakini siyo wakubwa wa dunia.