Jumatatu , 12th Apr , 2021

Mbunge wa Jimbo la Makete, Festo Sanga ametoa mchango wake katika bunge la Bajeti lililokuwa linaendelea Jijini Dodoma na ameainisha mambo manne muhimu kuhusu sekta ya michezo.

Mbunge wa Jimbo la Makete, Festo Sanga akizungumza na Waandishi wa Habari.

1.Kuondoa kodi kwenye vifaa vya michezo (Nyasi bandia ili serikali na wamiliki wa viwanja watandike nyasi.Jezi,mipra n.k kwaajili ya mashule na taasisi za michezo).

2.Kujenga shule za Michezo(football) za Kikanda (Special school kama ilivyokuwa Makongo chini ya Kipingu).

3.Makampuni ya kubashiri michezoni yadhamini Ligi kwasababu yanafaidika na michezo hasa mpira wa miguu nchini(Itungwe sheria itakayosimamia hili kwa lazima,pia makampuni yanayotaka kudhamini ligi yapungiziwe kodi ili vilabu vyetu vipate fedha).

4.Wawekezaji walindwe (wanaowekeza Simba na Yanga na vilabu vingine) Serikali isiruhusu watu kuwashambulia wawekezaji bila utaratibu wakati mchakato wote upo wazi na unabaraka zote za Mkutano Mkuu wa Simba na Yanga).

Simba ipo vitani ikipambania rekodi ya Africa, lazima tuwape nafasi wafanikishe jambo lao sio kuwachanganya na mambo madogo madogo ambayo yanazungumzia ndani ya Mikutano halali ya timu.

Hata Yanga ipo kwenye michakato ya uwekezaji, tukiendelea kuruhusu watu wa kuwavuruga wawekezaji kama (GSM) tutabaki palepale tulipodumu kwa miaka 100.