
Kikosi cha Serengeti Boys
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amesema, kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Bakari Shime kitakaa siku saba kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Korea Kusini kushiriki katika mashindano hayo ambayo yatasaidia kuendelea kukuza vipaji vya vijana hao.
Alfredyamesema, licha ya kukuza vipaji vya vijana hao lakini pia kwa upande wa wachezaji hao yatawasaidia kuweza kuonesha vipaji vyao na hata kuonekana kwa maskauti ambao watawatafutia timu kubwa zaidi.