Alhamisi , 26th Jan , 2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dokta Hassani Abbas wametembelea ofisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa jijini Dar es Salaam na kufanya kikao kazi na watumishi wa mfuko huo.

Mhe. Mchengerwa amefafanua kwamba Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria na imeanza kuwezesha wasanii kimitaji ili kuboresha maisha yao.

Aidha,  amesema  wiki ijayo Serikali itatoa mikopo ya awamu ya pili  baada ya Ile ya mwanzo iliyotolewa mwishoni mwa mwaka jana.

Ameongeza kuwa katika tukio hilo pia Serikali itapokea mdundo wa taifa na vazi la Taifa kutoka kwenye Kamati za kitaifa alizoziteua kufanya kazi hizo.