Ijumaa , 3rd Jul , 2020

Serikali  imeeleza kuridhishwa na uwekezaji mkubwa unaofanywa na viwanda vitatu mkoani Kilimanjaro kwa kuwekeza zaidi ya bilioni 190 na kutoa  ajira  kwa watanzania zaidi ya 8,000.

Waziri Angellah Kairuki

Hayo yameelezwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Mhe. Angellah Kariuki baada ya kufanya ziara ya kikazi katika viwanda vya Harsho wilaya ya Hai, kiwanda cha kutengeneza vinywaji laini cha Bonite Bottlers na kiwanda cha kutengeneza sukari cha TPC.

 Amesema Serikali  itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na wa nje wanaowekeza hapa nchini.

Wamiliki na viongozi wa viwanda hivyo mkoani Kilimanjaro wamebainisha aina tofauti ya changamoto katika viwanda vyao zikiwemo changamoto za maeneo, wataalamu kutoka nje ya nchi pamoja na uwepo wa mamlaka nyingi zinazofanya kazi zinazofanana.