Jumapili , 24th Dec , 2017

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein ametoa zawadi ya kiwanja kwa kila mchezaji wa Zanzibar Heroes pamoja na shilingi milioni tatu kwa kila mchezaji.

 

Dkt.Shein ametoa zawadi hizo katika hafla ya kuwapongeza wachezaji wa Zanzibar Heroes baada ya kufanya vizuri katika michuano ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA.

"Mmeonyesha kwamba mnaweza soka katika michuano ya CECAFA, kama serikali inabidi tuwatunuku zawadi jumla mko 33 wachezaji pamoja na viongozi wa timu, kwahiyo natoa pesa shilingi milioni tatu kwa kila mchezaji na viongozi wenu pamoja na kiwanja kwa kila mchezaji na kiongozi, na viwanja vyote vitakuwa sehemu moja mtaanzisha kijiji chenu",amesema Rais Dkt.Shein

Zanzibar Heroes walimaliza katika nafasi ya pili katika michuano  ya CECAFA, huku wakiwa na rekodi nzuri baada ya kumtoa bingwa mtetezi Uganda pamoja na kuwafunga ndugu zao Kilimanjaro Stars.