Simba wamkabidhi kazi Dkt. Tulia Ackson

Alhamisi , 10th Jan , 2019

Kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi kati ya Simba SC dhidi ya JS Sauora ya Algeria, Simba wememtangza Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kuwa mgeni rasmi.

Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.

Mchezo huo wa kundi D utapigwa Jumamosi hii kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kuanzia saa 10:00 jioni.

Taarifa ya Simba kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa Naibu huyo Spika amekubali na amethibitisha kuwa atakuwepo uwanjani kuwaongoza mashabiki wa Simba na wapenda soka kwa ujumla.

Wapinzani wa Simba JS Sauora wanatarajiwa kufika nchini leo saa 4:00 usiku tayari kwa mchezo huo ambapo kesho Ijumaa watafanya mazoezi kwenye uwanja wa taifa ambao utatumika kwenye mchezo.