Jumatatu , 21st Dec , 2020

Michuano ya kombe la shirikisho nchini kwa msimu huu inataraji kuendelea mwishoni mwa juma hili kwa michezo 32 ya mzunguko wa tatu ambapo vigogo vya soka nchini, Bingwa mtetezi wa kombe hilo klabu ya Simba, Yanga na Azam vikitaraji kucheza kati ya tarehe 25-27 mwezi huu.

Cedric Kaze, Sven Vandenbroeck, George Lwandamina

Bingwa mtetezi wa kombe hilo Wekundu wa msimbazi Simba ataianza kampeni ya kutetea kombe hilo kwa kucheza dhidi ya Maji Maji ya mkoani Ruvuma, Yanga kucheza na walima Arizeti klabu ya Singida United ya Mkoani Singida ilhali Azam kucheza na Magereza FC ya mkaoni Shinyanga.

Kutokana na ratiba hiyo kutoka usiku wa kuamkia hii leo inafanya mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya Yanga dhidi ya Ihefu ya jijini Mbeya kurudishwa nyuma, badal ya kuchezwa tarehe 26 mwezi huu sasa utachezwa tarehe 23 mwezi huu kwenye dimba la sokoine jijini Mbeya.

Wsindi wa michezo hiyo watafanikiwa kufuzu hatua inayofuata ya 32 bora inayotaraji kuchezwa kuanzia mwezi ujao.