Jumatatu , 2nd Mei , 2022

Klabu za Karia Koo Simba na Yang azote zimeondoka Jijini Dar es salaam leo asubuhi Mei 2, 2022. Yanga imeemda mkoani Kigoma na SImba imeelekea mkoani Lindi, ikiwa ni maandalizi kuelekea michezo yao ya ligi Kuu inayofuata.

Simba na Yanga zimeondoka Dar es salaam baada ya kucheza mchezo wa dabi ya Kariakoo Jumamosi Aprili 30. 2022.

Timu hizi zilicheza mchezo wa Dabi ya Kariakoo wa Ligi Kuu Jumamosi iliyopita April 30, 2022. Mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu 0-0, katika Dimba la Benjamini Mkapa Dar es salaam.

Klabu ya Yanga ambao ndio vinara wa Ligi wakiwa na alama 54 wameelekea mkoani Kigoma ambako watacheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting katika uwanja wa Lake Tanganyika Mei 4, 2022. Ruvu Shooting ndio wenyeji wa wa mchezo huu na wameupeleka mchezo huu Mkoani kigoma ikiwa ni sehemu ya kanuni inayowapa nafasi ya kuchugaa michezo miwili kucheza kwenye viwanja huru tufauti na viwanja vyao vya nyumbani.

Kwa upande wa Simba wameondoka Dar es salaam kwa njia ya ndege kupitia Mtwara na kesho Mei 3, 2022 watacheza dhidi ya Namungo FC uwanja wa Ilulu mkoani lindi.