
Haji manara akifunga kamba za viatu vya Clatous Chama.
Hilo limebainishwa na msemaji wa timu hiyo Haji Manara ambapo ameweka wazi kuwa kwasasa wao ni timu kubwa hivyo kila mchezo wanauchukulia kwa ukubwa na nidhamu ya hali ya juu.
''Tumewakumbusha wachezaji yaliyotokea mwaka jana na tumewaambia ukubwa wetu unatakiwa kuonekana uwanjani, hivyo mchezo dhidi ya Mashujaa tunauchukulia kama mchezo mwingine wowote'', amesema Manara.
Manara amesisitiza kuwa wao ni mabingwa watarajiwa wa Afrika hivyo kila kombe lililopo mbele yao wanachukulia kwa umuhimu mkubwa kwani wanataka kubeba mataji yote wanayoshiriki.
Simba kesho inashuka dimbani kucheza Mashujaa ya Kigoma kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya kombe la shirikisho nchini. Msimu uliopita Simba ilitupwa nje ya michuano hiyo ya Green Worriors ya Dar es salaam.