Simba yazidi kuisogelea Yanga, mbio za ubingwa VPL

Jumatano , 21st Apr , 2021

Mabingwa wa Tanzania bara klabu ya simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa katika dimba la kaitba huko Bukoba mkoani kagera.

Mshambuliaji wa Simba Luís Miquissone akishangilia baada ya kufunga goli

Mabao ya wekundu wa msimabazi Simba yamefungwa na Luís Miquissone dakika ya 13 na Chris Mugalu dakika ya 24. kwa ushindi huu Simba inafikisha alama 55 ikiwa ni tofauti ya alama mbili na vinara wa ligi Yanga wenye alama 57, wakati Kagera Sugar wanasalia nafasi ya 15 wakiwa na alama 27.

Michezo mingine ya VPL iliyochezwa leo, mchezo wa mapema ulichezwa Saa 8:00 Mchana klabu ya Ruvu Shooting iliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Mwadui FC  mchezo uliochezwa katika dimba la Mabatini mkoani Pwani, kwa ushindi huo Ruvu wanafikisha alama 37 wakiwa nafasi ya sita kwenye msimamo, na Mwadui wanaendelea kuburuza mkia katika nafasi ya 18 wakisalia na alama 16.

Na klabu ya Mbeya City imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Polisi Tanznaia kweye mchezo uliochezwa mjini Moshi, Kilimanjaro ktika dimba la Ushirika. Bao pekee la mchezo huo limefungwa na Kibu Denis dakika ya 52 na kuipa Mbeya City alama zote tatu, kwa mujibu wa msimamo Mbeya City inafikisha alama 24 wakipanda kwa nafasi moja kutoka ya 17 hadi 16, wakati Polisi wapo nafasi ya 9 na alama 34.