Alhamisi , 10th Oct , 2019

Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema wameipokea vizuri droo ya Kombe la Shirikisho na kwamba wanawamudu wapinzani wao Pyramids ya kutoka nchini Misri.

Yanga na Pyramids

Yanga imeangukia katika kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuondolewa katika hatua ya pili ya Klabu Bingwa Afrika na Zesco United ya Zambia, ambapo imepangwa na matajiri wanaokuja kwa kasi kutoka nchini Misri, Pyramids FC wakianzia nyumbani.

"Tunawamudu, kwanza Pyramids ni timu mpya ina miaka 11 tu na tunafahamu kuwa msimu uliopita mpaka kufikia walipo walimaliza nafasi ya tatu", amesema Hassan Bumbuli.

"Ni timu yenye uwekezaji mkubwa na ina pesa nyingi sana lakini pamoja na uwekezaji huo sisi tunaangalia kiwango cha uchezaji uwanjani", ameongeza.

Yanga itaanzia nyumbani kucheza na timu hiyo, Oktoba 27 katika Uwanja wa Taifa kabla kurudiana Novemba 3 nchini Misri.