
CEO wa Simba Barbara Gonzalez, Clatous Chama na Mwana FA
Katika picha hiyo chama ameandika Once a lion always a ? kisha akaacha sehemu ya kuweka jibu. Swali hilo linamaanisha (Simba siku zote atabakiwa kuwa ?).
Kwenye 'comment' moja ya watu waliojibu ni Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez ambaye ameweka emoj ya ishara ya kunyoosha mikono ambayo hutambulika kama heshima au kukubaliana na kitu.
Pia Mbunge wa Muheza ambaye pia ni shabiki mkubwa wa Simba SC, Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA, amejibu kwa kuweka emoj za Simba pamoja na ishara ya nguvu.
Kiungo huyo raia wa Zambia anatajwa kuwindwa na wapinzani wa Simba SC klabu ya Yanga, ambapo hadi sasa mkataba wake na Simba umebakiza miezi 7 umalizike lakini bado hajaripotiwa kama ameongeza mkataba.