Jumamosi , 14th Aug , 2021

Klabu ya Simba huenda ikapata pigo kubwa kufuatia nyota wake Clatous Chota Chama kuondoka msimbazi huku Luis Miquissone naye akikaribia kusajiliwa na mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri.

Luis Miquissone (Kushoto) na Clatous Chama (Kulia) wakiteta jambo katika moja ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Pigo kwa Simba linatokana na mchango mkubwa wa nyota hao wa kimataifa ambao wamekuwa sehemu kubwa ya mafanikio katika kufunga na kutengeneza nafasi za mabao kwa misimu kadhaa waliyokuwepo kikosini.

Katika mabao 78 ambayo Simba wamefunga msimu uliopita wachezaji Clatous Chota Chama na Luis Miquissone wamehusika kwenye mabao 42 yaliyofungwa na klabu ya Simba msimu uliopita.

Clatous Chota Chama amehusika kwenye mabao 23 (kufunga na asisti) wakati Luis Miquissone alihusika katika mabao 19(kufunga na asisti).

Kwa kuiweka sawa, Chama na Miquissone walikuwa na mchango wa asilimia 53.85 ya mabao ya Simba msimu uliopita.