
Akitangaza kikosi hicho,Kocha Mkuu wa Tanzania Hemed Suleiman Morocco amesema baadhi ya nyota wameachwa kwa ajili ya kwenda kuunda kikosi cha Tanzania chini ya umri wa miaka 20 kinachojiandaa na michuano ya kufuzu Afcon kupitia kanda ya CECAFA
''kikosi ambacho nimekiita nakiamini na anaimani watafanya vizuri katika mchezo huo ambao utakuwa mgumu kwa timu zote mbili huku amejaribu kuongeza wachezaji wengine ndani ya kikosi hicho ili kuongeza nguvu zaidi katika kikosi hicho kutokana na kuwaacha baadhi ya wachezaji wake''Amesema Morocco
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Afisa Habari wake Cliford Ndimbo amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kutoa hamasa kwa kikosi hicho ili kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa.
Mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya Nigeria unataraji kuchezwa Jumamosi ya Oktoba 29-2022 nchini Nigeria huku mshindi wa jumla akitaraji kufuzu kwa fainali za Afcon chini ya umri wa miaka 23 zitakazofanyika nchini Morocco mwaka 2023.