
(Kikosi cha timu ya taifa ya soka la Ufukwenu Tanzania 2021)
Baada ya mchezo huo wa ufunguzi, Tanzania itashuka dimbani tena leo saa 10:30 jioni kucheza dhidi ya Comoros kwenye mchezo wa pili wa siku ya Ufunguzi na endapo itapata alama nyingi basi itafuzu hatua ya mtoano inayofuata.
Tanzania ipo kundi B na timu za Mozambique na Comoros wakati wenyeji Afrika Kusini wapo kundi A na timu za Angola, Madagascar na Visiwa wa Seychelles.
Michuano hiyo imeanza kutimua vumbi Jumatano ya Jana Alhamisi Novemba 17 na kutaraji kutamatika Jumapili ya Novemba 21, 2021.