Jumamosi , 28th Jun , 2014

Baada ya kumaliza kwa kufungana mchezo mmoja mmoja katika fainali mbili zilizotanguliwa kabla ya fainali ya tatu ambayo iliahirishwa kutokana na giza kuingia katika uwanja wa Spider Gymkhana jijini Dar es salaam kesho mzizi wa fitina unakatwa

Wachezaji wa timu za ukanda wa Temeke na Kinondoni wakichuana katika michuano ya BBall Kitaa

Hatimaye mchezo wa tatu wa fainali ya mpira wa kikapu michuano ya BBALL KITAA unatarajia kurindima hapo kesho baada ya kuahirishwa Jumapili iliyopita kutokana na giza kutanda katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salam

Ambapo mratibu wa michuano hiyo Karaban Karaban amesema fainali hiyo itakayozikutanisha timu za ukanda wa Temeke, kanda ya mashariki ya kwanza na ukanda wa Kinondoni 'kanda ya Magharibi ya tatu itakuwa ya kipekee kutokana na ubora wa timu hizo na pia ubora wa mchezo huo unatokana na umuhimu wake kwakuwa mchezo wa kesho ndio mchezo ambao utaamua bingwa mpya wa michuano hiyo ambayo lengo lake kubwa ni kurudisha mpira wa kikapu mitaani huku walengwa wakubwa wakiwa ni vijana wadodo na watoto

Nao manahodha wa timu hizo za Temeke kanda ya Mashariki ya kwanza na Kinondoni kanda ya Magharibi ya tatu Murshid Mudricat na Ashraf Harun kila mmoja ametamba kuibuka na ushindi hapo kesho