Jumanne , 4th Oct , 2022

Ripoti kutoka nchini England zinaripoti kuwa kocha wa Manchester United Eric ten Hag yupo tayari kumruhusu mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo kuondoka klabuni hapo kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari 2023 kama wakipata ofa sahihi ya kumuuza mchezaji huyo.

Cristiano Ronaldo amecheza dakika 207 za EPL msimu huu kwenye michezo 6

Ripoti zinadai kuwa ten Hag amefikia uamuzi huo kutokana na presha kubwa anayokumbana nayo baada ya kutomchezesha mchezaji huyo kwenye mchezo wa Manchester Dabi dhidi ya mahasimu wao Manchester City, mchezo ambao Manchester United ilinyukwa mabao 6-3.

Nafasi ya Ronaldo kwenye kikosi cha The Red Devils msimu huu chini ya kocha Eric ten Hag imekuwa ndogo kwani amecheza michezo 6 tu ya Ligi kuu huku akiwa ameeanza mchezo mmoja pekee na michezo 5 ametokea benchi kama mchezaji wa akiba, kwa ujumla Ronaldo amecheza dakika 207 tu za EPL na amefunga bao 1.

Ronaldo mshindi mara 5 wa tuzo ya mcheaji bora wa Dunia alitaka kuondoka klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu, lakini Ten Hag alizuia mchezaji huyo asiondoke lakini kwa sasa anakumbana na ukosoaji mkubwa kwa kutompa muda mwingi wa kucheza na anatuhumiwa kumkosea heshima gwiji huyo wa soka.