
Tukio la kifo cha Mchezaji Ismail Khafan katika dimba la Kaitaba
Kesho Jumamosi Desemba 10, 2016 kutakuwa na mchezo maalumu wa kirafiki utakaozikutanisha timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara Mbao FC na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni utakuwa ni maalumu kwa ajili ya kutoa heshima kwa marehemu Ismail Khalfan - mchezaji wa timu ya vijana Mbao aliyefariki dunia Desemba 4, mwaka huu
Ismail alifariki uwanjani wakati akiiitumikia timu yake ya vijana kwenye mchezo wa Ligi ya Vijana ya TFF U20 dhidi ya Mwadui, uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera.
Waratibu wa mchezo huo wamepanga kukusanya mapato katika mchezo huo kwa ajili ya rambirambi na pole kwak familia ya kijana Ismail Khalfani.
Ismail Khafan (Kulia) akishangilia bao dakika chahe kabla ya kifo
Pia mchezo huo unatumika kama sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara kwa timu hizo.