
Rais wa TFF Wallace Karia
Kupitia taarifa yake maalum ya kufunga mwaka TFF, imesema moja ya mafanikio makubwa kwa mwaka huu ni makombe ambayo yameletwa nchini na timu za taifa ile ya vijana U17 (Serengeti Boys) pamoja na ya wanawake.
Imetaja makombe hayo ni yale mawili ya Serengeti boys ubingwa wa CECAFA walioupata mwezi April nchini Burundi pamoja na COSAFA walioupata Desemba hii nchini Botswana.
Katika mafanikio hayo TFF pia imeitaja timu ya taifa ya wanawake ya 'Kilimanjaro Queens' kwa kutwaa ubingwa wa CECAFA pamoja na timu ya taifa ya wanawake 'Twiga Stars' ambayo ilitwaa ubingwa wa Jumuiya ya Afrika mashariki.
Kwa upande wa vilabu TFF imetambua mafanikio ya klabu ya Azam FC kuwa mabingwa wa klabu bingwa Afrika mashariki maarufu kama Kombe la Kagame. Pia shirikisho hilo limeeleza mafanikio ya Simba kufika hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika.