
(Msemaji wa Mtibwa Sukari, Thobias Kifaru.)
Kifaru amesema:
''Lipo tatizo kubwa, nitazungumza lakini inawezekana watanitafsiri vibaya, lakini nataka kusema kuwa sisi bado hatujapiga hatua, bado tuna undugu undugu badala ya kujali kazi, sasa ukiweka undugu kwenye kazi huwezi kupata mafanikio, utaleta makundi makundi ambayo baadae hayawezi kujenga na kamwe hayaleti umoja sana sana wanaleta matokeo mabaya''.
''Tumekuwa na makocha wengi sana wakizawa sisi Mtibwa, lakini walikotupeleka siko, tumeamua kumsafirisha Joseph Omog kwa ndege maalum kutokea Cameroon, kwa lengo la kusema kwamba huyu hana rafiki, hana mjomba, hana kaka hana dada, anachojua ni kazi tu hivyo yeye atakachojali ni kuona kuwa mtu anauwezo ndio atampa nafasi.''
''Sasa sio sijui huyu mtoto wa mjomba, huyu mtoto wa binamu lazima acheze, hatupati mafanikio makubwa katika soka letu, sasa waliopewa dhamana wasiingie huko, hilo ni tatizo linalopelekea kutowaamini wazawa''
Kifaru ameyasema hayo alipokuwa anafanya mahojiano maalum na kipindi cha michezo cha KIPENGA cha East Africa Redio kinachoruka kila siku saa 2:00-3:00 usiku.