Jumamosi , 26th Aug , 2017

Timu ya TMT imefanikiwa kurejesha furaha kwa mashabiki zake kwa kuwapashika Mchenga BBall Stars kwa pointi 80-79 mchezo wa nne kati ya mitano katika fainali ya Sprite BBall Kings uliyopigwa kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Kutokana na matokeo hayo timu ya TMT imeweza kusimamisha ubingwa uliokuwa unategemewa na Mchenga BBall Stars kwa siku ya leo kuweza kumaliza mchezo huo lakini kwa bahati mbaya bahati ya ushindi haikuwa upande wao na kupelekea TMT kuwa sare na mpinzani kwa kushinda mechi mbili na kupoteza mbili katika jumla ya mechi tano za fainali hizi za Sprite BBall Kings.

Pamoja na hayo, mechi ya leo iliweza kuonyesha utofauti na ufundi mkubwa kutokana na timu zote mbili kupaniana na kusababisha kumaliza mchezo kwa tofauti ya pointi moja.

Mchenga na TMT zitakutana tena Septemba mbili (Jumamosi) ya mwaka huu kucheza game 5 ambapo mchezo huo ndiyo utakoweza kuamua mshindi ni nani kati ya wawili hao.